MREMBO TUNDA AKATA WATU WANAOMFOLLOW KWENYE ACCOUNT ZAKE
Mrembo
ambaye anafanya poa kwenye video za bongo Tunda, amewataka mashabiki
wake kuwa wakweli na kuacha unafiki, la sivyo wamuache kumfuata kwenye
mtandao wa kijamii.
Akiongea
kwenye kipindi cha PlanetBongo kinachorushwa na East Africa Television,
Tunda amesema anachukizwa na kitendo cha watu kujadili mambo
yasiyowahusu, pamoja na kuoneana wivu, na kuwataka wasimfollow kwenye
mitandao ya kijamii.
"Wanaonipenda
wanipende na wasionipenda waachane na mimi wasinifollow na kunijazia
coments za kipumbavu pumbavu, ila wanaonipenda wanifollow", alisema
Tunda.
Pia
Mlimbwende huyo ambaye ana mahusiano na msanii wa muziki wa bongo fleva
Young Dee, amesema anashangazwa na tuhuma anazopewa za kutumia madawa
ya kulevya, na bado analifanyia utafiti suala hilo.
"Kitendo cha kuniambia natumia unga mpaka leo sijui limeanzia wapi, hata sijui ila naendelea kufuatilia" alisema Tunda.
Kwa sasa mrembo huyo ameamua kurudi shule baada ya kuacha kwa muda mrefu na kujihusisha na sanaa
Comments
Post a Comment