CHECK PICHA MASTAA WA BONGO WALIOACHIWA WATOTO LAKINI HAKUNA NDOA



CHECK PICHA MASTAA WA BONGO WALIOACHIWA WATOTO LAKINI HAKUNA NDOA
rose_ndauka776Rose Ndauka
Mwandishi wetu, Risasi Jumamosi
MPANGO au matarajio ya kila mwanadamu ni kuishi katika uchumba, kuolewa kisha kupata watoto! Wapo ambao wamefanikiwa hilo, wapo ambao wamepata kwanza mimba baadaye wakaolewa lakini wapo pia waliopata mimba kabla ya ndoa kisha wakatofautiana na waliowapa, kila mmoja anaishi kivyake.
Katika ulimwengu wa mastaa wa kike Bongo, leo nakuletea baadhi ya mastaa ambao wamepata watoto lakini kwa namna moja au nyingine safari yao na waliowapa ujauzito haikufika mbali, ikavunjika. Wapo ambao walipata kabla na wengine baada ya ndoa.
Wengi wao huwanadi watoto hao mitandaoni kwa maneno mazuri wakionesha kwamba ndiyo faraja yao baada ya kuachana na wapenzi au waume wao;3
ROSE NDAUKA
Aliingia katika uchumba na Malick Bandawe. Wakafanikiwa kupata mtoto mmoja, uchumba ukayeyuka wakati wawili hao wakiwa katika mchakato wa kuelekea kwenye ndoa.snura
SNURA MUSHI
Amefanikiwa kupata watoto wawili; wa kike na wa kiume kwa baba tofauti. Wote wameingia mitini. Akapata mchumba mpya, naye wakamwagana kabla ya kufanikiwa kuolewa wala kuzaa.
ZUWENA MOHAMMED 'SHILOLE'
Ana watoto wawili wa kike ambao alizaa na wanaume wawili tofauti kwa nyakati tofauti. Kwa sasa wamemuachia chata ya watoto hao wa kike ambao anawadi mitandaoni.KAJALANAMWANAYE1
KAJALA MASANJA
Aliingia kwenye ndoa na Faraji Agustino akiwa tayari ameachiwa chata moja ya kike na Prodyuza, Paul Matthysse  'P Funk'. Bahati mbaya mumewe hakufanikiwa kuzaa naye, akafungwa kwa msala wa kutakatisha fedha haramu. Hadi sasa ana furaha kuwa na binti yake huyo.Hamisa-Mobeto-akiwa-na-mtoto-wake-aliyezaa-na-Majay                    (1)
HAMISA MOBETO
Alikuwa kwenye uchumba na bosi wa redio moja maarufu, akafanikiwa kupata mtoto mmoja na uchumba ukaishia hapo. Kila mtu yupo kivyake kwa sasa Mobeto anajifariji na chata yake ya kike aliyoachiwa._MG_4126
JENIFFER KYAKA 'ODAMA'
Inasemekana amezaa na kigogo mmoja ambaye ana familia yake. Inadaiwa kuwa kigogo huyo ameelekeza nguvu zake kwa mkewe hivyo Odama kubaki na chata yake ambayo anainadi kwenye mitandao ya kijamii mara kwa mara.uwoya4
IRENE UWOYA
Aliingia kwenye ndoa na mshambuliaji wa zamani wa Rayon Sports ya Rwanda, Hamad Ndikumana 'Katauti'. Akafanikiwa kupata mtoto mmoja wa kiume (Krish) kisha ndoa ikasambaratika na sasa anafarijika kwa kuachiwa kopi yake.
WENGINE
Masta wengine ambao kwa namna moja au nyingine wamezalishwa na kuachiwa watoto ni pamoja na Shamsa Ford, Faiza Ally aliyezaa na Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi 'Sugu', Siwema Edson (aliyekuwa demu wa Nay wa Mitego) na Riyama Ally ambaye ameachiwa chata ya kike.


Comments

Popular posts from this blog

WAREMBO KUMI WANAOTAZAMWA NA KUFATILIWA ZAIDI NA VYOMBO VYA HABARI AFRIKA MASHARIKI.

Teen kills father, opens fire on schoolyard in South Carolina